Katika hali inayohisiwa kuwa ni jaribio jingine la kuudidimiza na kuukandamiza Uislam Tanzania Mradi mpya unaojulikana "Ulinzi shirikishi kwenye Nyumba za Ibada" umesukwa huko Marekani na kukubaliwa na viongozi wa Usalama nchini Tanzania ili kupambana na Waislaam walio na Msimamo mkali.
Waislaam wa Tanzania waliokuwa na vidonda vya mauaji na mateso pamoja na kuswekwa kwenye magereza mbalimbali nchini humo sasa watakumbana na jaribio hilo ambalo wadadisi wa masuala ya kidini wanadai litafeli kutokana na ushiriki wa tasisi ya Bakwata isiyo na ridhaa ya waislaam walio wengi nchini Tanzania.
Kamati hiyo linalojumuisha watu sita au zaidi ya hapo ndani ya viongozi wa Misikiti mbalimbli nchini litakuwa na kazi ya kupitia na kuchunguza mwenendo na kufunga kamera za siri pasipo kujulikana waumini wanaosalia ndani ya msikiti.
Baadhi ya vyombo vya Habari vinayoegeme upande wa Serikali ya Tanzania inaupigia debe na kuwalaumu wadau wanaopinga hatua ya Serikali kuyaingilia Masuala ya ndani ya dini ya Kislaam na kudai kuw watu hao hawaitakii Amani Tanzania.
"Hata hivyo,baada ya Viongozi wa Kidini na Polisi kukubaliana kwa nia njema kuundwa kwa kamati hizo,kuna watu wamejitokeza wazi wazi kupinga wakidai ni kuingilia uhuru wa kuabudu na kutaka waumini waendelee na mambo yao na kamati hizo kubaki nje ya mfumo wa ulinzi".
"Wenye kuamini hivyo wakiongozwa na Katibu wa Jumuia ya Kislaam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda,wanasema hatua hiyo ni njama ya serikali kupitia Bakwata na jeshi la Polisi kukandamiza waislaam" ilidai Gazeti la Habari Leo.
Katika hatu nyingine inayonekana wazi kulipuzia maoni ya waislam na viongozi wakuu wa Waislaam Gazeti hilo limeongeza kusema: "Sisi tunadhani kuwa wanaopinga htua hiyo wanaunga mkono uvunjifu wa Amani na kamwe wasidhani Watanzania ni Wajinga wa kukubaliana na msimamo huo usio na tija kwao na hata kwa taifa kwa ujumla",ilisema sehemu ya tahariri ya Gazeti hiyo.
Gazeti la Habari leo likipoteza na kulificha lengo la kuundwa kwa Kamati hizo limedai kuwa ni kuepusha na kuzilinda Nyumba za Ibada kutokana na kulipuliwa kwa Mabomu na kuchomwa kwa Moto.
"Lengo ni kuhakikisha majumba hayo yanatumika ilivyokusudiwa/kuombwa,na si vinginevyo,na pale inapotokea watu au kundi la watu kwenda kinyume na hayo,basi hatua zichukuliwa sawia bila ajizi kwa kuamini kuwa wengi wa watanzania wanakerwa na tabia hiyo inayokithiri hivi sasa" Gazeti la Habari Leo.
Hatu hii mpya ya Serikali nchini Tanzania ni mfululizo wa kuwabana kuwaminya waislaam huko likisingizia kuzilinda nyumba za Ibada ikiwa na maana pamoja na Makanisa huko lengo likiwa ni Misikiti, na tayari baadhi ya mashekhe walioingia Mradi huo wmeshawachagua Kamati hizo tayari kufanya kazi na Maofisa wa Uslama nchini Tanzania ili kutaka kuwasaliti Ndugu zao.
Chanzo: Habari Leo
0 comments:
Post a Comment