Mauaji
yaliofanyika katika vijiji vya waislaam huko Kilindi vimenyamaziwa
kimya na Mashekhe wengi,na baadhi yao siku za nyuma walikuwa
wakijitokeza kwenye vyombo vya Habari na kutunisha misuli kwa masuala
yasio na manufaa kwa waislaam badala ya kuzungumzia madhila na mauaji
yaliofanywa na yanayoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini
Tanzania.
lakini kadhia hii ya mauaji ya
Kilindi na mahauji ya waislaam imenyamaziwa kimya na kufikia hatua kuwa
baadhi ya Mashekhe ukigusia kuuliza kadhia hizo wamekuwa wakali kwa
waislaam.
Ndugu yetu katika Iman hivi punde
alifanya mahojiano Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Baraza la
Wanazuoni Hey-At Ulamaa Tanzania Sheikh Mohamed Issa.
YALIYOMO JUU YA BAADHI YA MASHEIKH WA TANZANIA JUU YA KADHIA YA KILINDI.
Ndugu
zangu waislam suala zima la mji wa kilindi limekuwa gumu kupata habari
zake,na wala hatukuweza kuwasikia masheikh nchini tanzania
wakilizungumzia jambo hilo huku damu za waislam zikiwa zimemwagika.
Mahojiano yalifanyika hivi:-
Mwulizaji:-assalam alaykum sheikh mohammed issa.
Sheikh Mohamed Issa:-waalaykum salaam.
Mwulizaji:-niliikuwa nataka kujua kuhusiana na suala la kilindi sijui mmechukua hatua gani nyie viongozi.
Sheikh
Mohamed Issa:-mimi nimeingia leo nimetoka nje na mimi sio kiongozi,
wewe umenichagua mimi ukajua mm ni kiongozi,unajua mimi ninachokula kama
umenichagua mm kiongozi,kwanini wewe usifatilie wewe umechukua juhudi
gani.?
Mwulizaji:-sisi tunataka tujue kuna kauli gani kutoka kwenu nyie viongozi
Sheikh Mohamed Issa:- mimi sio kiongozi unajua mm nachokula,kwanza simu zetu zinarekodiwa,mnakaa nyie na wake zenunyumbani hamjui familia zetu zinakula nini alafu mnataka sisi tuwe wasemaji?
Mwulizaji:-sheikh
mohammad issa kumbuka mtume (Swal lahu aleyhi wasalam) amesema itafika
siku waislam watagombaniwa na makafiri kama chakula maswahaba wakauliza
kwa uchache wetu ya rasullallah mtume akasema mtakuwa wengi lkn wengi
wenu mtakuwa km takataka za mapovu ya bahari maswahaba wakauliza kwann
iwe hivyo mtume akasema mtasalitishiwa wahann maswahaba wakauliza nn
wahhan ya rasulla llah mtime akajibu ni kupenda dunia na kuchukia mauti.
Sheikhe
akauliza hii hadith ilikuwa makka au madinna akajibiwa madinna akasema
sisi hali tulokuwa nayo sasa ni hali ya makka hatuna nguvu kwa hiyo
hatuwezi kupambana na makafiri tunachofanya ni kuwaandaa waislam kwa
ajili ya siku za mbele.hata km sisi tukiwa tumefa.na kutoa mfano wa kisa
cha ammar bin yassir.
Kukawa
na majibizano makali na kukubali yeye ni kiongozi na wanawawekea
mawakili watu wa kilindi huku akijibu walouliwa allah ndio anajua
kuhukumu.
Subhannallah hii ndio hali halisi tulonayo waislam tanzania.
Chanzo cha habari ni kutoka vyombo vya habari somalia.
Nov 12, 2013
Sheikh Mohamed Issa "mimi sio kiongozi wa kuulizwa mauaji ya Kilindi!"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment