Askari polisi wa Idara ya Upelelezi waliokamatwa wakati wakijaribu kuuza jino la tembo, wilayani Serengeti, wamefukuzwa kazi.
Kwa sasa wanatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani Bunda kujibu mashtaka dhidi yao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Fernandi Mtui
alisema askari hao walikamatwa usiku wa Oktoba 25 mwaka huu wakiwa na
raia mmoja mkazi wa Bomani, mjini Mugumu.
Kamanda Mtui alisema walikutwa wakiwa na jino la
tembo wakiwa katika harakati za kutafuta soko na kwamba walikuwa
wanatumia gari.
“Baada ya kukamatwa, washtakiwa walishtakiwa
kijeshi na baadaye kufukuzwa kazi ili wafikishwe katika mahakama ya
kiraia,” alisema Mtui.
Alitoa wito kwa askari na wananchi kuacha kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali na kwamba watakaokamatwa watashtakiwa.
Kamanda huyo alisema katu polisi watasita kuchukua hatua.
0 comments:
Post a Comment