Nov 25, 2013

FAHAMU MAAZIMIO YA KANISA JUU YA VAZI LA HIJABU.


TAARIFA YA MAAZIMIO YA KIKAO CHA UMOJA WA WAKRISTO TANZANIA-KATORO NA BUSELESELE KUHUSU AMANI YA NCHI KUFATIA VURUGU ZA KIDINI NCHINI. KILICHOKETI TR 06/11/012.


Rejea taarifa ya kipindi cha matukio cha tarehe 06/11/2012 R.F.A kitendo cha Shekh wa Zanzibar ambae ni katibu wa Mufti wa Zanzibar kumwagiwa Tindikali Usoni na kifuani akifanya mazoezi yake eti kwasababu aliitaka serikali kuwachukulia hatua viongozi wa uamsho wanao sababisha vurugu za kidini Zanzibar, na kufungwa kwa shule ya sekondari iliyoko Bagamo kwa muda usio julikana kutokana na sababu za vuruguza kidini.


Ni baadhi ya matukio yanayo fanya umoja wetu kukaa na kuipatia tahadhari serikari yetu inayo ongozwa na Mh,Raisi J.M.KIKWETE, japo kuna matukio mengi yaliyo kwisha kupita ambayo yanajulikana, kama vile kuchomwa kwa shule ya wasichana ya shauri tanga ya moshi na wao kuungulia katika mabweni wakiwa wamefungiwa kwa nje,uchomaji wa bucha za nyama ya nguruwe Dar es salam enzi ya Mh rahisi Mwinyi(ruksa), Uchumoji wa BIBILIA takatifu zinazo fikia 52 hadi sasa nk.

Tuna unga mkono Tamko la Mh, Raisi wetu Jakaya Kikwete alilo litamka hivi karibuni kuwa hakuna dini nchini iliyo na mamlaka juu ya dini nyingine”, dini zote ni sawa kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwakua serikali ya Tanzania haina dini.


Kwa kuzingatia haya yote hapo juu,kikao kilichokaa tarehe 06/11/012 kilijadili mambo mengi yenye nia ya kuhamasisha amani hadi kufikia maazimio yafuatayo:-


1. UVAAJI WA IJABU KTK SHULE ZA SERIKALI.


Kama kweli serikali ya Tanzania haina dini, sisi wakristo tunataka kuona shule na vyuo na taasisi za serikali zinavaa sare zake(uniform) bilakuongezea mitindo mingine ya kidini mfano, hijabu haitakiwi kuvaliwa pamoja na sare za shure/chuo nk. Maana ya sale/Uniform,ni(a) aina moja ya rangi na (b) aina moja ya mshono kwawasichana/wavulana(jinsi/jinsia tofauti).Vaeni kama jeshi na benki(angalia wana vyo pendeza)kwani kule Benki na Jeshi hakuna waisilamu? Mbona hakuna hijabu?



Sisi wakristo hatuoni kuwa ni vyema kuona mitindo ya kidini moja inaruhusiwa mashuleni wakati dini nyingine hairuhusiwi. Tunaishauri serikali iliondoe jambo hili haraka iwezekanavyo.



Kama suala hili lita endelea bila kukemewa na serikari tutajua serikali ina tuambia uwongo na ina kiuka katiba ya nchi inaposema kuwa serikari haina dini, hivyo kuanzia mihula ujao January 2013, kama serikari haitazuia hijabu kuvaliwa ktk shule za serikari,basi nasi tutaamua kuwashonea watoto wetu mikanda iliyo andikwa
“YESU NI BWANA” wa ende nayo shuleni wakiwa wameivaa".


Si mara ya kwanza kwa Viongozi wa Kinasara nchini Tanzania kupinga masuala inayowahusu waislaam walio wengi nchini,miaka ya nyuma Viongozi hao wa Kinasara walikwisha pinga Mahakama ya Qadhi kwa Waislaam wakidai kuwa Mahakama hiyo itasababisha ukikwaji wa Haki za Binadamu,na pia walipinga maoni ya waislaam kuwa Tanzania ijiunge na Umoja wa Nchi za OIC ambayo ni Muungano wa Nchi ya Kislaam na Kinasara.

0 comments:

Post a Comment