Aug 6, 2013

SWAUTUN NAQY KUZINDUA ALBUM

  • NI YA AMANI YA TANZANIA.
  • MGENI RASMI NI KAMANDA SULEYMAN KOVA,
  • WAISLAMU WATAKIWA KUHUDHURIA KWA WINGI.
Na mwandishi wetu wa munira.
Kikundi cha Swautun Naqii chenye makazi yake Temeke Vetenary jijini Dar es salaam,kinatarajia kufanya uzinduzi wa Album ya Qaswida inayojulikana kwa jina la AMANI YA TANZANIA.

Akiongea katika mahojiano maalumu na mwandishi wa blog hii Ustaadh Muhammad Muhiya amsema uzinduzi huo utafanyika siku ya IDD pili kuanzia saa nane katika viwanja vya mnazi Mmoja ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Suleyman Kova.

Ustaadh Muhiya alisema kwamba katika uzinduzi huo kikundi cha Swautin Naqy kitatambulisha kaswida zake sita ambapo alizitaja kuwa ni Amani ya Tanzania inayobeba Album,Mke mwema,Saluqalbi,Wagonjwa,Pongezi kwa akina baba na Pongezi kwa akina mama kaswida ambayo ilitokea kutamba katika miaka ya nyuma.


Akijibu swali la mwandishi wa munirablog aliyetaka kujuwa sababu ya kutunga Qaswida inayozungumzia Amani ya Tanzania,ustaadh muhiya alisema "Hii Amani tuliyopewa na ALLAH ni tunu kwenu,tukae tukitambua kwamba hatutakiwi kuichezea kwa namna yoyote,tunawajibika kuilinda kwa gharama yoyote,kwani ikituponyoka, kuipata tena itakuwa ngumu sana,sasa mimi ambaye nimejipa dhamana ya kufikisha ujumbe kwa njia hii ya tungo ya qaswida nikaona ni vyema nami nitoe mchango wangu juu ya Amani ya Tanzania.".mwisho wa kumnukuu.

Aidha kikundi hicho kinatarajia kufanya uzinduzi wa album hiyo katika mikoa ya Arusha,Mwanza na Singida mara tu baada ya uzinduzi wa siku ya Idd pili.

Ustaadh Muhiya alitowa wito kwa wazazi wa kiislamu na wasio kuwa wazazi kuhudhuria kwa wingi ukizingatia kwamba hakuna kiingilio,kwani maeneo haya ndiyo wanayotakiwa waislamu kuja kwa wingi na sio kwenda katika maeneo ambayo yatawaharibia ibada yao waliyoichuma kwa taabu ndani ya mwezi wa Ramadhan.

Vikundi mbalimbali vitakuwepo katika kuisindikiza album hiyo ikiwepo kikundi cha Firqatu ssalaam chini ya uongozi wa ustaadh Khamis Mshauri na madrasat Thanawiyyah ya Temeke ambapo vikundi vyote vitapiga Live.