Kiongozi wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania,
Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi mkoa wa Morogoro na kusomewa mashitaka matatu yanayomkabili.
Ponda alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi
waliokuwa na mbwa baada ya kupokelewa kutoka katika Viwanja vya Gymkhana
alipotua kwa helkopta majira ya saa tatu asubuhi akitolewa katika Gereza la
Segerea, jijini Dar es Salaam.
Makosa matatu aliyosomewa Sheikh Ponda na wakili wa serikali, Bwana Bernard
Kongola mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Richard Kabate ni ya
uchochezi na kutaka kuvuruga amani ambayo mtuhumiwa ameyakana.
Mawakili wa upande wa mtuhumiwa walikuwa Ignas Pungu na Bantalomeo Tarimo,
wakati upande wa serikali kulikuwa na Benedict Kongola, Gloria Rwakibalila na
Asnab Mhando.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Agosti 28 mwaka huu na mtuhumiwa amerudishwa
Segerea jijini Dar es Salaam
kwa usafiri ul
eule wa helkopta.