- SERIKALI YATANGAZA HALI YA HATARI,
- IDADI YA VIFO INATISHA,
- MUSLIM BROTHERHOOD YAAHIDI KUTORUDI NYUMA.
Na mwandishi wetu wa munira;
Katika hali ya kukandamiza haki na Demekrasia katika nchi ya Misri,kiongozi mkuu wa vuguvugu la Muslim Brotherhood nchini Misri,
Mohammed Badie amekamatwa na maafisa wa usalama kutoka makaazi yake eneo la
Nasr 'City', Mjini Cairo. Badie aliwekewa kibali cha kumkamata kwa tuhuma za
kuchochea ghasia na mauaji.
Hali ya hatari imetangazwa Misri huku serikali ikiendelea kuwawinda wafuasi
wa Brotherhood ambao wamepinga kuondolewa madarakani kwa Rais Mohammed Mosri.
Taarifa hiyo ina liamrisha pia jeshi kukisaidia kikosi cha polisi
"kutanzua mzozo unaotokea kote Misri."
Taarifa hiyo imetolewa wakati vikosi vya usalama vilikuwa vinashambulia makambi mawili kuwaondowa wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi kati kati ya mji mkuu wa Cairo.
Taarifa hiyo imetolewa wakati vikosi vya usalama vilikuwa vinashambulia makambi mawili kuwaondowa wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi kati kati ya mji mkuu wa Cairo.
Mohammed Badie amekua akiwaomba wafuasi wa Muslim Brotherhood kuandamana na
kuweka kambi zao mjini Cairo.
Hata hivyo alikwenda mafichoni tangu Julai 10. Jeshi lilivunja kambi hizo na
watu wengi waliuawa na kujeruhiwa
Kiongozi huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia na mauaji ya raia
wanane mahasimu wa Muslim Brotherhood.
Kukamatwa kwa Badie kunajiri siku kadhaa
baada ya mwanawe wa kiume Ammar kupigwa risasi na kuuawa katika maandamano
yaliyofanyika medani ya Ramses.
Vuguvugu hilo
limesema hatua ya kumkamata kiongozi wao hazitakandamiza wafuasi wake na kwamba
mamilioni wataendelea kupinga mapinduzi dhidi ya utawala uliochaguliwa
kidemokrasia.
Mrengo wa Brotherhood wa kisiasa, ambacho ni chama cha Freedom And
Justice umemtangaza Mahmoud Ezzat kuchukua nafasi ya kiongozi mkuu.
Ezzat ni Naibu mwenyekiti wa chama hicho. Wakati huo huo Serikali ya Misri imetangaza
siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia mauaji ya maafisa 25 wa polisi
katika Rasi la Sinai, hapo Jumatatu.
Wanamgambo wa kiisilamu wamelaumiwa kutekeleza mauaji hayo.Shambulio hilo lilifanyika katika mji wa Rafah ulioko mpaka na
Ukanda wa Gaza.
Wakati huo huo kumekuwepo na ripoti zinazotofautiana hii leo ambapo karibu watu 900 wameuawa wakiwemo mahabusu wa Brotherhood 37 ambao walifariki dunia wakipelekwa katika jela moja nje ya mji wa Cairo.Mamia ya wafuasi wa vuguvugu hilo akiwemo Naibu wake Badie, Khairat al-Shatir wamekamatwa tangu kuondolewa kwa Mohammed Mosri hapo Julai Tatu.
Hata hivyo baadhi ya wanachama wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bw Morsi wanasema idadi ya walofariki imefikia hadi 2,200 na wengine elfu 10 kujeruhiwa. sauti ya amerika haijaweza kuthibitisha idadi hizo zote zinazotolewa.
Mohammed Badie ambae amekamatwa.
Gari la polisi linasukumwa na kunagushwa kutoka daraja na waandamanaji karibu na kambi kuu la mkusanyiko mkubwa wa wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi katika wilaya ya Nasr City mashariki ya Cairo,
Afisa wa usalama abishana na mama mmoja anabeba fimbo katika eneo ambalo wafuasi wa rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi wamekusanyika katibu na Chuo kikuu cha Cairo, huko Giza, Cairo