- IMEANDAA KAMBI YA DINI KWA SIKU MOJA,
- KUFUTURU PAMOJA,
- VIJANA WA KIISLAMU WAHAMASISHWA KUSHIRIKI.
Na mwandishi wetu wa munira
Kundi la Skauti la Shule ya Qiblatain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es salaam,linatarajiwa kufanya sherehe za kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.
Kiongozi mkuu wa kundi hilo Mwalimu Omar Mavura ameipasha munirablog kwamba kilele cha hafla hiyo kitafanyika tarehe nne ya mwezi wa nane mwaka huu katika viwanja vya shule ya sekondari ya Qiblataini vilivyopo Kawe Ukwamani.
Amesema wameandaa kambi hiyo ya siku moja itakayofanyika tarehe tatu mwezi wa nane na kukhitimishwa tarehe nne ya mwezi huo itakayoambatana na tukio la kufuturu pamoja na watu mbalimbali ikiwemo masheikh viongozi wa kiserikali na baadhi ya wabunge.
Miongoni mwa mambo yatakayofanyika katika kambi hiyo ni pamoja na kutolewa mafunzo ya Skauti yatakayoambatana na nasaha za kidini kutoka kwa wanazuoni na viongozi mbalimbali.
"Washiriki ni vijana wote wa Kiislamu wenye umri wa miaka kumi hadi kumi na nane,kwani lengo letu ni kuwajenga kiukakamavu na kuwajenga kiimani"alisema Alhaj Omar ambaye pia ni mwalimu katika Shule ya Qiblatain.
Aliongeza kwa kusema kwamba kwa wazazi watako kuwa tayari kushiriki kwa vijana wao basi wawasiliane na viongozi wa kundi hilo kwa namba 0655 75 66 88 (mwalimu omar),
0684 11 11 17 mwalimu muhiddin.
Kundi la Skauti la Qiblatain liliwahi kupata tuzo ya Dunia ya kuwa kundi bora la Skauti Duniani kwa mwaka 2007.
HII NI SEHEMU YA MATUKIO MBALIMBALI YANAYOFANYWA NA KUNDI BORA LA SCOUT DUNIANI MWAKA 2007.
HAPA MABINT WAKAKAMAVU WA QIBLATAIN SCOUT WAKIPITA KATIKA MILIMA YA HATARI.
"POLE BABA YETU',NDIVYO WANAVYOONEKANA KUSEMA WANASKAUTI WA QIBLATEN WALIPOWATEMBELEA WAGONJWA KATIKA MOJA YA HOSPITALI ZA JIJINI DAR ES SALAAM.
MBALI YA KUJIFUNZA UKAKAMAVU,LAKINI PIA WANATIMAZA WAJIBU WA KUSWALI POPOTE WAWAPO.
HAPA WANASKAUTI WA QIBLATAIN WAKIWA KATIKA MAFUNZI YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO.
HAPA NI MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KUWAFARIJI WATOTO WALIOPO KATIKA GEREZA LA WATOTO UPANGA DAR ES SALAAM.
HAPA WANAONEKANA WAKIWA KATIKA MAFUNZO YA KUMSAIDIA ALIYEJERUHIWA.