Kidavashari alisema usiku huo wa tukio, Suzana alikuwa amelala peke yake nyumbani kwake, jirani na nyumba walimolala wake wa mwanawe, Paul Charles, ambao ni Maria Kanyungiro na Maria Nsabi.
Ilidaiwa kuwa wakati mke wa kwanza, Maria Kayungiro akiwa chumbani kwake, alisikia mama mkwe akikimbia kutoka nyumbani kwake akienda kwenye nyumba walimokuwa wamelala wakweze, huku akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema ‘mama nakufa nakufa... nisaidieni.’
Mama mkwe wake alipofika katika nyumba walimolala wakweze, alisukuma kwa nguvu mlango wa chumba alichokuwa amelala mke wa pili, Maria Nsabi na kuingia chumbani huku akihema kwa hofu na akiendelea kupiga mayowe.
Kamanda Kidavashari alidai kuwa watu hao, ambao hawakufahamika mara moja wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, walikuwa wakimfuata kwa nyuma wakimfukuza.
Inadaiwa wauaji waliingia ndani ya chumba hicho, wakitumia mwanga wa kurunzi na kumkuta Suzana amejilaza na mke huyo wa pili wa mwanawe kitandani.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kidavashari, wauaji hao walianza kumshambulia Suzana kwa mapanga na hatimaye kumchinja
0 comments:
Post a Comment