May 5, 2014

MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA SHEIKH HASSAN ILUNGA







MWILI WA MARHUUM SHEIKH HASSAN ILUNGA UKISHUSHWA KATIKA KABURI LAKE.

Maelfu ya Waislamu leo hii wamejitokeza kwa wingi kumzika mwanaharakati mahiri Sheikh Hassan Ilunga.

Sheikh Ilunga alifariki usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari kwa muda mrefu.

Maandalizi ya maziko yake yalifanyika katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa Jijini Dar es salaam.

Katika dua hiyo iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na Shuura ya Maimamu,ilihudhuriwa na Waislamu wengi waliofurika msikitini huku wengine wakikosa nafasi ndani na kulazimika kuswali nje.

Viongozi mbalimbali wa Kiislamu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara  na visiwani Zanzibar walishiriki.

Makamu wa wa kwanza wa Rais wa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa ni kiongozi pekee wa Serikali aliyeshiriki maziko hayo kuanzia hatua ya mwanzo hadi mwisho.

Maziko yake Sheikh ilunga yaligusa hisia za wengi kiasi cha watu wengine kushindwa kujizuwia na kutokwa machozi.

Akiwahutubia maelfu ya Waislamu walioshiriki maziko hayo makaburini,Sheikh Ally Bassaleh aliwataka Waislamu kuiga ujasiri wa Sheikh Ilunga huku akisema kwamba wingi wa watu walioshiriki msiba huo ni ishara ya wazi kwamba Sheikh ilunga alikuwa anafanya kile ambacho waislamu wanakitaka.

Sheikh Ilunga enzi za uhai wake alikuwa ni mwiba mkali kwa Serikali ya Tanzania kiasi kwamba ilitangaza kumtafuta kwa madai ya kufanya uchochezi uchochezi.

Aidha mwaka jana serikali kupitia Jeshi la Polisi lilitangaza kwamba atakaye kutwa na kanda,cd na dvd za Sheikh Ilunga atakamatwa.

Hii ilitokana na ujasiri aliokuwa nao Sheikh Ilunga juu ya kupinga mfumo kristo unaowakandamiza waislamu nchini Tanzania.

Allah amrehemu Sheikh Hassan Ilunga na alifanye kaburi lake kuwa ni kiwanja miongoni mwa viwanja vya Peponi,amiin.
 
 MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIZA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AKITOKA MSIKITI WA KICHANGANI NA KUINGIA KATIKA GARI KUELEKEA MAKABURI YA MWINYIMKUU.
WAUMINI WAKIELEKEA MAKABURINI
 WAUMINI WAKIWA NJE YA MSIKITI WA KICHANGANI BAADA YA KUKOSA NAFASI NDANI.
 MAKAMU WA WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR PAMOJA NA PROF IBRAHIM LIPUMBA WAKIWA ENEO LA MAKABURI YA MWINYIMKUU.
 



HILI NDILO KABURI LA MARHUUM SHEIKH ILUNGA

0 comments:

Post a Comment