Apr 25, 2014

MSF: Waislamu Myanmar wanahitaji misaada

Wafanyakazi wa jumuiya za kimataifa za misaada ya kibinadamu wanasema kuwa Waislamu wa Rohingya nchini Myanmar ambao wamekusanywa katika kambi za wakimbizi wanahitaji misaada ya dharura ya chakula na dawa.

Wafanyakazi wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) wanasema kuwa watu kadhaa wamefariki dunia na kwamba makumi ya watoto wanazaliwa katika mazingira mabaya kwenye kambi hizo za Waislamu wa Myanmar tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Ripoti zinasema kuwa maelfu ya Waislamu wa kabila la Rogingya huko Myanmar wanasumbuliwa na uhaba wa chakula, maji na huduma za afya katika jimbo la Rokhine kutokana na hujuma zinazoendelea kufanywa na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya jamii ya Waislamu.

Vilevile mamia ya wafanyakazi wa jumuiya za kimataifa za misaada ya kibinadamu wamehamishwa kutoka Sittwe, makao makuu ya jimbo la Rokhine baada ya kushambuliwa na Mabudha.

Maelfu ya Waislamu wameuawa katika hujuma za Mabudha wenye misimamo mikali huko Myanmar.

0 comments:

Post a Comment