Feb 24, 2014

TUJIUNGE NA VIKUNDI VYA UMOJA ILI TUBORESHE MAISHA YETU-UMATADA






 HAWA NI VIONGOZI WA UMATADA MARA BAADA YA KUCHAGULIWA TENA KUONGOZA.
Wananchi wameshauriwa kujiunga na vikundi vya umoja ili kuboresha maisha yao.

wito  huo umetolewa na katibu mkuu wa UMOJA WA MAENDELEO YA WAKAAZI WA TANGA WAISHIO DAR ES SALAAM ndugu Omar Rashid Shemsigwa
.
Shemsigwa ameyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurudi tena madarakani kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ulifanyika katika ukumbi wa shule ya Al Haramain ya Jijini Dar es salaam.
Amesema "kuna fursa nyingi wazipatazo wananchi pindi wanapojinunga na vikundi vya maendeleo fursa ambazo hazipatikani unapokuwa nje ya kikundi".

"Ndugu mwandishi moja ya fursa zilizopo katika kikundi chetu ni pamoja na kukupatia faraja pale unafiwa,sisi tunakupatia shilingi laki tano,mchele kilo mia moja,sukari kilo kumi na mafuta lita kumi:.

Aliendelea "kusema tunayafanya haya kwa kufahamu kwamba msiba ni tukio gumu na linakuja ghafla,sasa tunapotoa msaada katika wakati huo,inakuwa tumemfariji mfiwa kwa kiasi kikubwa sana:Mwisho wa kumnukuu.

Alizitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na kusafirisha mwilini wa marehemu hadi kijijini kwake kwa mazishi,kuwalipia wanachama wao au ndugu wa karibu wa wanachama wao gharama zote za matibabu maadamu mgonjwa huyo anatibiwa katika Hospitali ya Serikali.

Aidha umoja huo unamiliki ardhi heka Hamsini zilizopo Handeni Mkoani Tanga.

Wakati huo huo wanachama wa UMATADA wameurudisha madarakani uongozi wote wa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika jana.

Akitangaza matokeo hayo,Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ambaye pia ni mlezi wa chama hicho mzee Ayoub Shebuge alisema,waliopiga kura wlikuwa ni wanachama 145 ambapo Abdul Ramadhan Mswati alitetea kiti cha uenyekiti kwa kupata kura 134,wakati Juma Hassan Shebuga alitetea nafasi yake ya umakamu mwenyekiti kwa kupata kura 135.

Omar Rashid Shemsigwa alirudi katika nafasi yake ya ukatibu mkuu kwa kuzoa kura 135.

Nafasi ya Naibu katibu mkuu ilirudi tena kwa Muhammad Rupatu aliyepata kura 124 na mweka hazina aliendelea kuwa Issa Mhilu aliyejinyakulia kura 132.

Umoja huo wenye makao makuu Mbagala Zakhem kwa sasa unawanachama hai 222. 

 MWENYEKITI WA UMATADA ABDUL RAHMAN MSWAKI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU

 KATIBU MKUU OMAR RASHID  SHEMSIGWA AKISOMA AGENDA ZA MKUTANO MKUU
 AL HAJ ABDALLAH OMAR SABAYA AKISOMA DUA KWA NIABA YA WAISLAMU


 PETRO SHUNDA AKISOMA DUA KWA NIABA YA WAKRISTO.

BAADHI YA WAJUMBE WAKIFUATILIA TAARIFA YA MWAKA 2013 IKIYOSOMWA NA KATIBU MKUU.
 KATIBU WA TUME YA UCHUGUZI AL HAJ ABDALLAH SABAYA AKITANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI.


 MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI AMBAYE PIA NI MLEZI WA CHAMA HICHO MZEE AYOUB AKIWA WA KWANZA KUPIGA KURA.

 WAJUMBE WAKIINGIZA KURA KATIKA MABOX

MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI AKITANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI

MKUTANO ULIMALIZIKA KWA WANACHAMA KUPATA CHAKULA MAALUM.

0 comments:

Post a Comment