Ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, imelaani vikali
mashambulizi yalotekelezwa mnamo Jumapili na watu wenye silaha dhidi ya
vijiji 8 katika majimbo ya Adamwa na Borno, nchiniNigeria, na kuwaua
watu zaidi ya 150.
Ripoti zinasema watu wapatao 65 waliuawa katika vijiji 7 kwenye
jimbo la Adamwa, huku wengine 90 wakiuawa katika kijiji cha Izge kwenye
jimbo la Borno.
Wakazi wengi sasa wameyakimbia makazi na vijiji vyao kwa kuhofia mashambulizi zaidi. Ravina Shamdasani ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Feb 19, 2014
Ofisi ya haki za binadamu yalaani mauaji vijijini Nigeria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment