Feb 21, 2014

Machafuko CAR yumkini yakaenea katika nchi jirani

Kuna uwezekano wa kupanuka machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hadi katika nchi jirani na taifa hilo. 

Hii ni katika hali ambayo, wanamgambo waasi wa Kikristo wa Anti-Balaka, wamevishambulia vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini humo, suala lililopelekea kuibuka mapigano kati ya pande mbili.
Habari zinasema kuwa, makumi ya watu wamepoteza yao katika mapigano hayo. Siku moja kabla wanamgambo hao wa Anti-Balaka walimiminika mabarabarani huko Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo, kupinga ripoti ya ikulu ya rais iliyowataka Waislamu kurejea mjini humo.

 Hii ni katika hali ambayo wapiganaji wa waasi wa Seleka wametangaza kuwa, hawatoondoka katika maficho yao na kwamba, hawana nia ya kuanzisha mapigano ndani ya nchi hiyo ya katikati mwa Afrika. 

Wakati huohuo gazeti la Daily Telegraph linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa, utendaji mbovu wa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani umesababisha kuendelea kwa mauaji dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:

Post a Comment