Katika hatua kadhaa zinazochukuliwa kuondoa msongamano wa magari barabarani katika jiji la Dar es Salaam, mikakati iko mbioni ya kuleta mabasi yatembeayo juu ya maji.
Katika kutimiza azma hiyo, Kampuni ya Transevents Marketing ya Tanzania kwa kushirikana na Kampuni ya Dutch Amphibious Transport Vehicles (DATV) ya Uholanzi zimeanza mchakato wa kuleta usafiri wa mabasi ya abiria yenye uwezo wa kusafiri nchi kavu na majini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Transevents, Peter Nzunda anasema teknolojia hiyo ya mabasi ya nchi kavu na majini (amphibious) ina lengo la kupunguza tatizo la foleni kwenye barabara za Dar es Salaam hususan katikati ya jiji kwa kuwa mabasi hayo huweza kupita nchi kavu na majini.
Hii ina maana kuwa hata katika maeneo yenye barabara zisizo nzuri au zenye tope, magari hayo huweza kupita hivyo kutosababisha foleni kama ambavyo hutokea sasa katika baadhi ya maeneo hasa mvua zinaponyesha na kuharibu barabara.
Anasema mbali na lengo hilo, mabasi hayo yatatumika kama vivutio vya utalii kwa kufanya utalii wa baharini ambao kwa Tanzania haujashika kasi, licha ya sehemu kubwa ya nchi kuzungukwa na maji.
“Mpango huo wa mabasi ya nchi kavu na majini unalenga kutoa ushawishi kwa watu wa kundi la kati ambao wanatumia magari binafsi waegeshe magari yao na kutumia usafiri huu ambao utakuwa wa hadhi yao na unaokidhi haja kwa ubora wake,” anasema Nzunda.
Nzunda aliongezea kusema “Lengo ni kujenga maegesho ya magari maeneo mbalimbali kandokando ya bahari, watu wataegesha magari yao na kupanda mabasi yatakayopita majini kwenda Posta na baadaye kurejea kwa utaratibu huohuo na kuyachukua magari yao tena kwenye maegesho
0 comments:
Post a Comment