Dec 11, 2013

Ikhwan yatoa sharti la kukubali kura ya maoni

Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imesema itakubali matokeo ya kura ya maoni ya katiba mpya ya nchi hiyo kwa sharti kwamba washiriki wa zoezi hilo wafikie milioni 35. 

Sharti jingine lililotolewa na harakati hiyo ni asilimia 75 ya washiriki wa kura hiyo ya maoni kuipigia kura ya ndio. 

Amru Durakh, Mkuu wa Kamati ya Mahusiano ya Nje ya chama cha Uhuru na Uadilifu ametangaza kwamba, Ikhawanul Muslimin hado haijatoa uamuzi wa mwisho kuhusu kushiriki au kususia kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri.

Hii ni katika hali ambayo, Katibu Mkuu wa chama cha Kiislamu cha Jihad ametangaza kuwa watasusia kura hiyo ya maoni na kuwataka wananchi wasishiriki kwenye zoezi hilo.  

Kura hiyo ya maoni kuhusiana na katiba mpya ya Misri itafanyika mwezi ujao wa Januari mwaka 2014.

0 comments:

Post a Comment