Dec 21, 2013

MTOTO ACHINJWA KAMA KUKU


 

MTOTO wa Diwani wa Mkangano, Estoni Kimwelu (CCM), na mfanyakazi wa ndani, Sista Nyilenda (17), wameuawa na watu wasiojulikana.

Tukio hilo la kinyama lililotokea juzi saa nane mchana, eneo la Tazara, Tunduma, wilayani Momba, ambapo mtoto huyo, Kalibu Kimwelu (6),   alichinjwa shingoni kama kuku, na mfanyakazi huyo akinyongwa hadi kufa kwa kutumia waya wa televisheni uliokuwepo sebuleni.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Barakael Masaki, alisema watu waliotenda unyama huo walivamia nyumbani kwa diwani huyo ambaye alikuwa shambani na mke wake Tumaini Yohana (29) anayefanya kazi ya ukatibu muhtasi katika halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma akiwa kazini.

Alisema baada ya kutekeleza unyama huo, watuhumiwa waliiba mabegi mawili makubwa yaliyokuwa na nguo mbalimbali ambazo thamani yake haijajulikana.

Kamanda Masaki, aliongeza kuwa miili ya marehemu ilikutwa ikiwa sebuleni, na polisi walianza uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwashikilia watoto watano wa mke mkubwa wa diwani huyo.

Waatu kadhaa wana shikiliwana jeshi la polisi.

Kamanda Masaki alisema uchunguzi wa awali unaonyesha mauaji hayo yametokana na ugomvi wa muda mrefu wa kifamilia kati ya mke mkubwa na mdogo.

Alisema familia ya mke mkubwa imekuwa ikidai kutelekezwa na kunyimwa mali ambazo zinaaminika zimekuwa zikiinufaisha familia ya mke mdogo.

0 comments:

Post a Comment