Nov 15, 2013

WAISLAMU Watakiwa Kumtegemea ALLAH




 SHEIKH ABDALLAH HARUON.

Imeelezwa kwamba kumtegemea ALLAH ndiyo njia pekee itakayo muokoa mja kutoka katika mitihani mbalimbali.

Hayo yapo katika khutba ya Ijumaa iliyotolewa hivi punde katika Msikiti wa Qiblaten uliopo Jijini Dar es salaam.

Akitafsiri khutba hiyo Imamu wa Msikiti wa Qiblatain Sheikh Abdallah Haroun Nyumba alisema,unapojenga moyoni kumtegemea ALLAH S,W hakuna dhara litakalo kukuta.

Huku akitoa mifano mbalimbali alisema"Nabii Ibrahiim A.S alihukumiwa kutoswa motoni,lakini alipotoswa katika moto mkubwa ulioandaliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja,Nabii Ibrahim hakutetereka zaidi ya kumtegemea ALLAH na kwa hakika ALLAH alimnusuru huku makafiri na mushrikina wakipata khasara"

Aidha alisema kumtegemea ALLAH kunaenda sambamba na Ikhlaswi kitu ambacho kinapotea kwa waislamu siku hadi siku.

"Leo waislamu wengi wamekuwa na tabia ya kugombea kuongoza nafasi mbalimbali ndani ya Uislamu,lakini wanapopata madaraka hayo,hawafanyi kwa Ikhlaswi zaidi ya wao kutaka kujinufaisha,kwa mazingira haya si rahisi kupata mafanikio zaidi ya kupata fedheha"mwisho wa kumnukuu. 

Khutba hiyo iliandaliwa na kusomwa na sheikh Dokta Usamah Mahmoud ambaye ni mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri kilichopo Chang'ombe.

0 comments:

Post a Comment