Nov 20, 2013

Kesi Ya UAMSHO Yarudishwa Zanzibar.

Kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar imerudishwa tena Zanzibar.

Akiongea na munira blog mapema leo hii,Kaimu Katibu Mkuu Ustaadh Salum Amour amesema "nimekuja Mahakama ya Rufaa kufuatilia maombi yetu tuliyo yawasilisha miezi minane iliyopita,lakini leo mahakama imeamua kulirudisha shauri hilo mahakama kuu ya Zanzibar"

Akifafanua zaidi Ustaadh Salum Amour alisema,tokea viongozi wao wakamatwe na kuzuiwa dhamana sasa ni mwaka mmoja na wiki tatu.

"Dhamana ni haki ya raia kikatiba,lakini inasikitisha kuona kwamba mashtaka haya yanaendeshwa kisiasa zaidi na si kisheria,wale wale waliotunyima dhamana ndiyo tunarudishwa kwao kwa jambo hilo hilo,"alidai

Aliendelea kusema kwamba Jumuiya ya Uamsho ipo kisheria na imesajiliwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hati no 149 na miongoni mwa malengo yake ni kutetea na kupinga dhulma dhidi ya waislamu.

"Mbali ya kupinga dhulma,pia tunawasaidia yatima,tulitoa misaada katika ajali ya MV Spice,tumechimba visima viwili hapo hapo gerezani,tulitaka kujenga hospitali lakini serikali imezuwia kila kitu hadi hati ya kiwanja,kimsingi hatujatoka nje ya malengo yetu.alidai.

Aidha alisema iwapo shauri hilo litaendelea kuendeshwa kisiasa,basi wao watalipeleka shauri hilo kwa waislamu .

Akijibu swali la mwandishi wa munira blog aliyetaka kujuwa tetesi zilizopo juu ya Jumuiya hiyo kuhusishwa na chama cha siasa,Ustaadh Salum Amour aliyapuuza madai hayo na kusema hayana msingi.

"Kimsingi Uamsho haifungamani na chama chochote,ndiyo maana CUF wanatutuhumu sisi kuwapora wafuasi wao na CCM wana tutuhumu kuivuruga nchi,tungekuwa tunafungamana nao,madai haya yasingesikika".


Wakati huo huo Kaimu Katibu Mkuu wa UAMSHO amesema licha ya Sheikh Azzan Kurejea hivi karibuni kutoka nchini India kwa matibabu,hali za viongozi wa Uamsho waliopo katika gereza la kiinua mguu ni mbaya.

"Ukiwatazama unaweza ukawaona wana Siha mzuri ,lakini hali zao ni mbaya,kwani wapo katika eneo lisilo na usafi,chumba chao kina ACID masaa Ishirini na nne,hawaoni nje na wamepoteza uwezo wa kubaini harufu",alidai kwa masikkito sheikh salum amour wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi ofisini leo hii.

0 comments:

Post a Comment