Oct 4, 2013

MASHEIKH Wauliwa KENYA


Kuna taarifa kwamba Sheikh Ibrahim Rogo ameuawa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari ni kwamba sheikh Ibrahim na wenzake wameuawa kwa kupigwa Risasi usiku wa kuamkia leo.

Inasemekana kwamba mauaji dhidi ya masheikh hao yamefanyika wakati masheikh hao wakitoka katika ibada ya swala ya Asubuhi Masjid Musa mjini Mombasa.

Sheikh Ibrahim Rogo ndiye aliyekuwa mrithi wa Sheikh Aboud Rogo aliyeuwa kwa kupigwa risasi na wanaodaiwa kuwa ni maafisa wa usalama nchini kenya mapema mwaka jana.

Hivi karibuni nchini kenya kumekuwa na mauwaji dhidi ya masheikh hali ambayo inatia wasiwasi wa amani nchini humo.

Hadi sasa polisi nchini kenya hawajasema lolote.

Munira blog imefanikiwa kunasa picha za mauwaji hayo,na inawaomba radhi wasomaji kwa hisia zozote zitakazo tokana na Picha hizo.










0 comments:

Post a Comment