Jun 5, 2013

KULINGANIA UMOJA NI WAJIBU WETU.
  • ASHANGAZWA NA KANISA KUIJIBIA SERIKALI.
  • ASEMA KUPINGA DHULMA SIYO KUVUNJA UMOJA. 
Imeelezwa ya kwamba suala zima la kunadi umhimu wa umoja miongoni mwa wananchi wa Tanzania ni suala ambalo halihitaji mjadala.

Hayo yameelezwa na Sheikh Nassor Muhamad Majid alipokua akijibu swali la muandishi wa habari aliyetaka kujuwa msimamo wa waislamu kuhusu kauli ya serikali inayotolewa mara kwa mara ya kusisitiza umoja  .

Alisema umoja hauna mjadala,kwani kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya uislamu,umoja ni wajibu wetu sisi waislamu miongoni mwetu napia ni wajibu wetu kuwa na umoja hata kwa wasio waislamu.

Lakini akatanabaisha ya kwamba umoja huu haumanishikwamba sisi waislamu tukubali kudhulumiwa,vile vile kupinga dhulma siyo tafsiri ya kuvunja umoja,ikitokea serikali au madhehebu yakaelewa kinyume cha hivyo itakuwa falsafa ya umoja haikueleweka vizuri.

Aliendelea kusema kwamba waislamu hawana ugomvi na wakiristo,bali ugomvi walionao waislamu ni dhidi ya serikali kunakotokana na wao serikali kuikandamiza jamii ya kiislam.

Alitolea mfano wa hivi karibuni,mara baada ya kanisa kupigwa bomu kule Arusha na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa,kiongozi mmoja mwandamizi wa Serikali (bila ya kutaja jina) alinukuliwa akisema kwamba wahusika ni magaidi (Waislamu) na kasema kwamba muhisika alikuwa amevaa balaghashia (kofia) lakini baada ya kukamatwa kwa anayesaidikiwa na kubainika si muislamu jambo hilo limekuwa kimya kabisa kama kwamba halikutokea.

"Napenda niwaambie waandishi wa habari ya kwamba,siyo suluhisho kwa serikali kutumia mabavu dhidi ya waislamu au jamii yoyote inayopaza sauti kutokana na dhulma wanayofanyiwa".mwisho wa kunukuu\

Sheikh Nassoro hakusita kuonyesha masikitiko yake juu ya tabia ya taasisi za kanisa kuijibia serikali pale waislamu wanapotoa malalamiko yao dhidi ya serikali.
Pichani sheikh Nassor Muhammad Majid (IBAADH) akiongea na waandishi wa habari,kushoto kwake ni Sheikh Abdallah Bawazir ambae pia ni Mwalimu bobezi wa Somo la Hadithi katika msikiti wa Qiblatain na Msikiti wa Kipata iliyoko katikati ya jiji la Dar es salaam.

Picha na habari kwa mujibu wa mwandishi wa munirablogspot.

0 comments:

Post a Comment