Feb 19, 2015

Umoja wa Mataifa wasikitishwa na utekaji nyara wa albino Tanzania

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania 
amesema watu wenye ulemavu wa ngozi wanastahili kuwa na haki sawa kama raia wote wa Tanzania.

Nchini Tanzania, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez ameelezea wasiwasi wake baada ya watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi, au albino, kutekwa nyara katika ukanda wa maziwa makuu nchini humo.
Akizungumza , Rodriguez amesema mtoto wa kwanza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka jana na hadi sasa hajapatikana na mnamo siku ya jumapili, mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja, Yohana Bahati, alitekwa nyara kwa msingi wa ulemavu wake wa ngozi, kwenye wilaya ya Chato, mkoa wa Geita.

Maiti ya mtoto Yohaba imepatikana jana kwenye msitu wa Biharamulo, na mama yake ambaye aliyejeruhiwa na watekaji nyara bado amelazwa kwenye hospitali ya Mwanza.


Rodriguez amesema, mwaka huu wa 2015 unaweza kuwa hatari kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwani ni mwaka wa uchaguzi, na vitendo vya uchawi vinavyolenga watu wenye ugonjwa wa ngozi vinaweza kutokezea.

Ameziomba mamlaka za serikali kuu na serikali za mitaa kuongeza bidii ili kuhakikisha utawala wa sheria na utunzaji wa haki za binadamu kwa watu wote.

Aidha amesisitiza kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanastahili kuwa na haki sawa kama raia wote wa Tanzania.

0 comments:

Post a Comment