Machafuko na mapigano ya hivi karibuni huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yamewaathiri pakubwa watoto nchini humo. Watoto katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wahanga wakubwa wa mashambulizi ya makundi yenye silaha.
Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Taasisi moja isiyo ya kiserikali ya Italia mjini Bangui amesema kuwa, huko nyuma watoto walikuwa wahanga wasio wa moja kwa moja wa machafuko yanayojiri Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini hivi sasa watoto hao wanalengwa moja kwa moja na machafuko hayo.
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) ulitangaza Disemba 30 mwaka jana kuwa waligundua vichwa vya watoto wawili vikiwa vimetenganishwa na mwili huku mwili wa mmoja wa watoto hao ukiwa umekatwa vipande vipande.
Wakati huohuo Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa mapigano ya kidini yanayoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamewalazimisha raia wa nchi hiyo karibu milioni moja kuyakimbia makazi yao.
0 comments:
Post a Comment