Maafisa wa jeshi la Uganda wamethibitisha kwamba kamanda wa kundi la
waasi la M23 la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Sultan Makenga
amejisalimisha na anashikiliwa na Uganda.
Hata hivyo maafisa hao
hawajaeleza bayana mahala kamanda huyo anashikiliwa kwa wakati huu.
Hatua hiyo ya kundi la M23 kutangaza kwamba linaweka chini silaha zake
na hapo siku ya Alhamisi kutangazwa kujisalimisha kwa kamanda wake
Sultan Makenga kwa maafisa wa Uganda kunachukuliwa kuwa ushindi mkubwa
kwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- FARDC.
Nov 12, 2013
Kamanda Makenge Akamatwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment