Nov 12, 2013

Siasa za kibaguzi na kikatili za Israel zazidi kulaaniwa

    ukubwa wa hati
Siasa za kibaguzi za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeendelea kulaaniwa vikali huko Palestina.

Taasisi moja ya kutetea haki za binadamu imekosoa na kulaani vikali siasa za kibaguzi za utawala huo ghasibu.

Kanali ya Televisheni ya Press TV imeinukuu taasisi  moja ya haki za binadamu katika mji wa Haifa ikizilaani siasa za kibaguzi na kimabavu za utawala haramu wa Israel.

Taasisi hiyo imetoa wito wa kuheshimiwa haki za binadamu za Wapalestina. 

Aidha taasisi hiyo imeitaka jamii ya kimataifa kuushunikiza utawala huo ghasibu, ili uhitimishe siasa zake za kibaguzi dhidi ya Wapalestina.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina yamesisitiza tena kwamba, njia pekee ya kukomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na maghasibu Wazayuni na kuhakikisha Wapalestina wanapatiwa haki zao ni kudumishwa mapambano ya muqawama.

0 comments:

Post a Comment