Jun 16, 2013

WAZAZI WATAKIWA KUWALEA NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA.
  • ASEMA HALI YA MAADILI NI MBAYA SANA,
  • NI MUONGOZO WA DINI PEKEE UNAOWEZA KUIONGOA JAMII,
Habari na mwandishi wa blog ya munira
Nasaha zimetolewa kwa wazazi wote nchini kuwalea na kuwasimamia watoto wao katika maadili mema ili kuwa na taifa lenye raia wema.

Nasaha hizo zimetolewa usiku huu na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Juma Duni Haji alipokuwa anawahutubia waislamu waliokusanyika katika hafla ya Maulid yaliyoandaliwa na Madrasat Hussein Shadhilii ya magomeni makuti jijini Dar es salaam.

Amesema Dunia ya sasa imetawaliwa na nguvu kuu tatu,alizitaja nguvu hizo kuwa ni nguvu ya uchumi,nguvu ya siasa na nguvu za kidini.

Amesema waliokuwa na pesa wanapigania waingie katika siasa ili wakamilishe malengo yao,na walio katika siasa wanataka pesa ili waishi vizuri.

Nguvu ya dini ni kubwa na ndiyo pekee ikitumika vizuri inaweza kuiokoa na kuiongoza jamii kuwa na maadili mema.

Dini zote zinaamrisha waumini wao kuwa wema na kuacha maovu,lakini utashangaa hao wanaofanya maovu ni waumini wa dini hizo hizo,hii ni ishara ya kwamba viongozi wa dini wanahitajika kuongeza kasi ya dhati katika hili. 

Alisema ya kwamba hali ya maadili imekuwa mbaya sana,kila kukicha watu wanalia juu ya mmomonyoko wa maadili,lakini ni vyema tukafahamu ya kwamba jukumu hili ni lenu mashekh kwa kushirikiana na wazazi.

"Leo mtoto wa kiislamu akikuwa,akasoma na akaowa hali ya kuwa bado yupo katika maadili mema,basi wewe mzazi au mlezi umshukuru mungu,kwani  watoto wa sasa wamezungukwa na mipapa na minyangumi ya maadili mabaya yanayochangiwa na viongozi"mwisho wa kumnukuu.

Alisema kwa fikra zangu viongozi wanachangia kumomonyoka kwa maadili,kwani kama viongozi (wa dini na viongozi wa familia ) wakitimiza wajibu wao vizuri,bila shaka yoyote maadili yatakuwa mazuri.

Mheshimiwa Juma Duni alikhitimisha nasaha zake kwa kuwataka wazazi wasijisahau kuwajengea uwezo wa heshima watoto wao pale aliposema "Tuwaandae watoto wetu ili wajiheshimu na kuheshimiwa,kwani hata sisi hadi kufikia umri huu na tukawa tunaheshimiwa ni kutokana na wazazi wetu kutuandaa vyema wakati wa utoto wetu"mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Juma Duni Hajj ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya maulid yalifanyika usiku huu katika viwanja vya Madrasat Hussein Shadhilii iliyopo magomeni makuti,jijini Dar es salaam .
Pichani juu Mheshimiwa Juma Duni Hajj ambaye ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,akiwahutubia waislamu waliohudhuria hafla ya maulid usiku huu maeneo ya magomeni makuti,jijini Dar es salaam,

0 comments:

Post a Comment