Jun 9, 2013

TAASISI YA ANNAHL TRUST FUND YAZINDUA SHINDANO LA BADRI.
  • LENGO NI KUKUZA MAARIFA YA WANAFUNZI.
  • WASHINDI KUIBUKA NA ZAWADI NONO. 
 Na mwandishi wetu wa muniramadrasablogspot.
Taasisi ya Annahli Trust Fund ya jijini Dar es salaa,leo hii imezindua shindano la vita vya badri katika ukumbi wa lamada uliopo ilalajijini  Dar es salaam.

Akiwahutubia wanafunzi wa elimu ya kati (sekondari) walihudhuria uzinduzi huo,mjumbe wa Taasisi hiyo Sheikh Khatwib Mussa alisema lengo la mashindano haya ni kukuza maarifa ya wanafunzi wa kiislamu ili waweze kujuwa historia ya vita vya badri na hekima yake sambamba na kuijuwa historia ya uislamu wao kwa ujumla.

Alisema vita (tukio la vita) vya badri lina mafunzo makubwa na mazito ambayo kama wanafunzi na waislamu kwa ujumla watayatilia maanani ni wazi watafaidka nayo.

Akifanya mahijiano maalumu na mwandishi wa blog ya munira muda mfupi baada ya uzinduzi huo,Sheikh Khatib Mussa alisema taasisi ya yake mbali ya kuwa na malengo kadhaa lakini pia inajishughulisha na kuendesha mashindano hayo katika kila mwezi wa ramadhan tokea mwaka 2006.

Aliwataja walengwa wa mashindano hayo kuwa ni wanafunzi wa kiislamu waliopo katika shule za sekondari kutoka wilaya zote za moa wa Dar es salaam.

Alisema kila wilaya inapambanisha wanafunzi wake waliokubali kwa kupitia shule zao,na kisha kila wilaya inatoa washindi watano bora ambao wataingia fainali itakayo wajumisha wanafunzi kumi na tano na khatimaye kupatikana mshindi.

Fainal hiyo inatarajiwa kufanyika ndani ya mwezi wa Ramadhan ya mwezi kumi na saba ambapo mbali ya kuwepo kwa zawadi kwa washiriki wa jumla lakini pia kutakuwa na zawadi maalum kwa washindi wa shindano hilo.

Sheikh khatwib alizitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na lapo top,Computer,Simu na Vitabu mbalimbali kwa mujibu wa fani ya mwanafunzi husika.

Aidha alisema mbali ya vitabu vya elimu ya kimazingira lakini pia watatoa zawadi kwa washindi kwa kuwapatia vitabu vya dini ambavyo taasisi ya Annahli wanahusika na kuvitafsir(kwa lugha ya kiswahili)  ikiwemo kitabu kikubwa na mashuhuri cha tafsir ya Qur aan ya Ibni Kathiir.

Akijibu swali la mwandishi wa muniramadrasa.blogspot  aliyetaka kujuwa ni kwa nini mashindano haya yafanyike mwezi wa Ramadhan badala ya miezi mengine,Sheikh Khatwib alisema "kila mtu ana utaratibu wa kumpokea mgeni,na mwezi wa Ramadhan ni mgeni muhimu kwetu waislamu,tukaona kwa kuwa muongozo wa waislamu (Qur aan) umeshuka ndani ya mwezi wa Ramadhan,basi ni bora nasi tumpokee mgeni wetu kwa kuendesha shindano hili ambalo linaanza leo na litamalizika Ramadhan ya mwezi kumi na saba siku ambayo kwa mujibu wa historia vilipiganwa vita vya badri ambavyo licha ya uchache wa waislamu wakiongozwa na Mtume Muhammad S.A.W lakini waliwashinda makafiri waliokuwa zaidi ya elfu tatu".mwisho wa kunukuu.

Mbali ya kuzitaja changamoto zinazoikabili taasisi ya Annahl kuwa ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa zawadi,hakusita kumshukuru mungu juu ya mafanikio kadhaa waliyoyapata yakiwemo kuwakutanisha wanafunzi wa kiislamu ngazi ya sekondari ambao mwishowe wanajenga umoja kwa misingi ya uislamu.

Kwa upande wake Omar Jabir Said ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Pugu anayesoma kidato cha nne,mbali ya kuishukuru Taasisi ya Annahli kwa kuwakutanisha na kuwaunganisha wanafunzi wa kiislam pia aliwapongeza kwa wazo lao la kuanzisha shindano hilo kwani linawapa nafasi ya kuwa na bidii ya kujisomea vitabu vya dini wakiwa mashuleni tofauti na hapo awali.

"Unajuwa sisi wanafunzi wa shule za serikali,hatuna muda wa kutosha wa kujisomea vitabu vya dini zaidi ya kujisomea vitabu vya masomo mengine,lakini kwa mashindano haya sasa tunahamasika kujisomea sana vitabu vya dini ili kujiweka vizuri kielimu na kimashindano na hii ndiyo iliyoifanya shule yetu ya pugu mwaka jana kuwa washindi wa pili wa shindano hili",mwisho wa kumnukuu. 

Alieleza masikitiko yake ya kuwa katika shule 72 za manispaa ya ilala ni wanafunzi wa shule zisizo zidi 17 ndizo zinazo shiriki shindano hili,alishauri hamasa iongezwe kwa walimu walezi wa shule mbalimbali,huku akiwaasa wa waandaaji watimize ahadi zao wanazo ahidi.

Naye bi Zainabu Mustwafa mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Taifa Islamic iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam,yeye alisema,"tumenufaika sana na uwepo wa shindano hili,kwani mwisho wa yote tunaijuwa vizuri historia ya vita vya badri,tunafahamu nani na nani alifariki na tunapata ujasiri wa kutosha kwa maana woga unatuondoka",mwisho wa kumnukuu.

Alishauri shindano hili pia lipelekwe mikoani ili wanafunzi wenzao wafaidike na maalumati hayo.

 Mjumbe wa Taasisi ya Annahli Trust Fund Sheikh Khatwib Mussa akitoa hutuba ya ufunguzi wa shindano la badri kwa wanafunzi wa kiislamu wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es salaam,uliofanyika leo hii katika ukumbi wa Lamada uliopo Ilala jijini Dar es salaam.

 

0 comments:

Post a Comment