Jun 11, 2013

KUACHA MAASWI NI KATIKA UCHAMUNGU.
Mabalaa na majanga yanatokana na kukithiri kwa maasi.

 Na mwandishi wa munirablog


Waislamu nchini wameelezwa ya kwamba tabia ya kujizuwia,kujivua na kujitenga na maaswi ni katika mambo ya kiucha mungu anayo yaridhia Allah mtukufu.


Hayo yalisemwa hivi karibuni na Sheikh Abdallah Haroun Nyumba ambaye ni imamu wa Masjid Qiblatain uliopo kariakoo jijini Dar es salaam.

Akiwasomea Qiswa cha ISRAA na MIIRAJ baada ya swala ya maghrib waumini waliohudhuria katika msikti huo alisema,kwa mujibu wa mambo yalivyo,kufanya ibada siyo kazi ngumu,bali kazi ngumu ni kuacha maasi yaliyokuzunguka ili uwe na nafasi ya kupata radhi za mwenyeezi.

Alizidi kusema ya kwamba,hali imekua ni kinyume kabisa,leo watu wamezama katika dimbwi la maasi kana kwamba hakuna sheria au muongozo wa namna ya kuishi.Aidha  mbali ya wao wenyewe kufanya maasi lakini pia wanatoa ushirikiano mkubwa katika kuwasaidia wanaofanya maasi,

Akitolea mfano alisema,"leo fundi mjenzi anakubali kupewa kazi ya kujenga Guest House (nyumba ya wageni) hali ya kuwa anajuwa fika nini kitakachofuata baada ya ujenzi huo kumalizika,kufanya hivi ni kusaidia maasi"mwisho wa kunukuu.

Akinukuu maneno ya Imamu Ghazal alisema,"Dunia ina nusu mbili,nusu ya kwanza ni kuacha makatazo (kuacha maasi ya Mungu na mtume wake Muhammad S.A.W ) na nusu ya pili ni kufanya Twa'a (ibada) na huko kuacha maasi ndiyo ucha mungu.'

Aliwanasihi waumini wa kiislamu kujitenga na maasi yote kwani,mabalaa,majanga na gharka mbalimbali zinazotokea hapa duniani,chanzo chake ni kukithiri kwa maasi.

Mwezi wa Rajab ni mmoja katika miezi minne mitukufu ambao waumini wa kiislamu wanaamini katika mwezi huu (wa Rajab ) kuwa mtume s.a.w alifanya safari ya ISRAA na MIIRAJI na hatimaye kupitia safari hiyo akafaradhishiwa swala tano,hivyo misikiti mbalimbali husoma kisomo cha miiraji inafika mwisho wa mwezi wa Rajab,

 
 Picha juu.Sheikh Abdallah Haruon Nyumba akisoma Qiswa cha Israa na Miiraj katika msikiti wa Qiblatain,hivi karibuni



 Sehemu ya waumini wa msikiti wa Qiblatain,wakifuatilia kwa makini kisomo cha miiraji kikichosomwa na sheikh Abdallah Haruon,hivi karibuni.
Picha na mwandishi wa munirablog.


0 comments:

Post a Comment