- ASEMA KUTOA SIRI NI HATARI KWETU NA KUNAONDOSHA HESHIMA NA UJASIRI.
Hayo yamesemwa na sheikh Abbas Juma (ambaye kitaaluma ni Daktari katika Hospitali ya serikali mkoani mbeya).alipokua akitoa mada ya vita vya badri kwa washiriki wa shindano la vita vya badri lilifunguliwa leo hii katika ukumbi wa lamada uliopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Alisema "waislamu tumekosa nguvu (tofauti na wingi wetu na sifa yetu) dhidi ya maadui wa uislamu,sababu kubwa ni sisi kutokutunza siri zetu",mwisho wa kunukuu.
Akizungumza kwa uchungu,alisema,leo tunaweza kukaa na kupanga mikakati mbalimbali ya dini yetu,lakini baada ya muda utaisikia mikakati hiyo ikisemwa katika hutuba,katika makongamano na yamezaagaa mitaani,unabaki kushangaa imekuwaje siri hii ipo nje,haya ni matatizo makubwa sana ambayo yanatusibu sisi waislamu.
Aliendelea kusema jamii yoyote haiwezi kupata heshima na ujasiri kama hawatakuwa na nidhamu na utamaduni wa kutunza siri.
Alitolea mfano katika mchakato wa vita vya Badri,alitumwa mzee mmoja kuupeleleza msafara wa Mtume s,a,w,yule mzee alipokutana na Mtume na kumuuliza anatokana na nani,mtume alimjibu sisi tunatokana na maji.
Mtume alitumia hekima pasipo kuongopa wala kumpa siri ya msafara wao,mafunzo ambayo leo hii tumeyatupa nyuma ya migongo yetu alisema kwa masikitiko makubwa.
Alitoa mfano wa pili kwamba,swahaba Hudhaifa ndiye sahaba pekee,ambae mtume s.a.w.alimpa majina ya wanafiki wasiopungua sabini tena akiwajuwa waziwazi,lakini hakuwahi hata mara moja kuvujisha siri hiyo.
Alionyeshwa kushangazwa na tabia hiyo pale aliposema,"siri zetu tunazitowa kuwapa maadui wetu,lakini na sisi hatuna ujanja wala uwezo wa kung'amua siri zao,hii ni khatari kubwa,mwisho wa kunukuu.
Sheikh Abbas Juma alikuwa anawasilisha mada ya badri ambayo ilikuwa itolewe na sheikh Shaaban Mussa ambaye alidharurika.
Shindano hilo limeaandaliwa na Taasisi ya Annahli Trust Fund ya jijini Dar es salaam ambapo litafikia kilele chake mwezi 17 Ramadhan Inshaallah kwa washindi kukabidhiwa zawadi mbalimbali.
Doctor Sheikh Abbas Juma,akiwasilisha mada ya vita vya badri kwa washiriki wa shindano la vita vya badri,lililofunguliwa leo hii jijini Dar es salaam.
Pichani juu,baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es salaa ambao pia ni washiriki wa shindano la Badri,wakimsikiliza kwa makini mtoa mada Doctor Abbas Juma,alipowasilisha mada hiyo leo katika ukumbi wa lamada jijini dar es salaam.
Picha na habari na mwandishi wetu wa blog ya munira.
0 comments:
Post a Comment